National News

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUMBAKA MTOTO NA KUMWAMBUKIZA VVU

Tarehe: 29 Oct, 2023


Mahakama ya wilaya ya Iringa imemhukumu kifungo cha maisha mara mbili, fidia ya shilingi Milioni 25, faini ya Milioni 5 pamoja na viboko 11 Mzee Selemeni Gwabuga Selemani mwenye umri wa miaka 78 aliyekuwa anaishi eneo la Idod, Isimani na alikuwa akiishi jirani na familia ya mtoto huyo
Hukumu hiyo inakuja Baada ya kukutwa na hatia ya Makosa matatu ya Kubaka mtoto mwenye umri wa Miaka 11 na Kumuambukiza Virusi vya Ukimwi kwa makusudi huku akijua kuwa yeye ni muathirika na anatumia dawa za ARVs.

Akisoma Hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa amesema mtuhumiwa amekutwa na hatia ya Kubaka bila kuacha shaka kwamba alimbaka mtoto wa miaka 11 na kumuambukiza mtoto huyo ukimwi Kwa makusudi.

Kesi hiyo ilisimamiwa na waendesha mashtaka wa serikali Nashon Saimon pamoja na Burton Mayage na Ilikuwa na Mashahidi wanne akiwemo Daktari aliyempima Mtoto huyo na Kuthibitisha kuwa alikuwa ameingiliwa na kusababisha kuambikizwa virusi vya Ukimwi.

Aidha katika Vielelezo vilivyopelekwa mahakamani hapo Vilionyesha kuwa Mtuhumiwa Seleman aligundulika kuwa na Virusi vya Ukimwi mwaka 2016 katika kituo Cha afya Cha Mahuninga na Kuanza kutumia dawa za kufubaza virusi hivyo yaani ARVs

Akiongea mahakamani hapo mwendesha mashtaka wa serikali Burton Mayage aliiomba mahakama kutoa adhabu Kali Kwa Mtuhumiwa Kwa Sababu ugonjwa aliomuambukiza mtoto huyo hauna tiba na Itadumu katika kipindi chote cha Maisha ya mtoto huyo lakini pia amemuathiri kisaikolojia mtoto huyo.

Mzee selemani alipopewa nafasi ya kujitetea aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu Kwasababu afya yake sio Nzuri na Umri wake ni mkubwa kwani ana miaka 78.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab