National News

RAIS SAMIA ASISITIZA UTUNZAJI MAGARI YA WAGONJWA

Tarehe: 28 Oct, 2023


Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amewataka watendaji wa mikoani kutunza magari ya kubeba wagonjwa na vifaa tiba walivyopatiwa kwani Serikali imetumia fedha nyingi kuhakikisha maboresho katika sekta ya afya yanawafikia wananchi.

Rais Samia ameyasema hayo leo Oktoba 28, 2023 wakati wa uzinduzi  wa magari ya kubebea wagonjwa pamoja na magari ya usimamizi 369 kwa niaba ya kundi la jumla la magari 989 na vifaatiba 388 ambavyo vimetolewa nchi nzima.

"Naomba mkatunze vile vifaa ni ghali mmesikia mabilioni ya pesa yametumika kununua kwa hiyo naomba mkatunze,"- Rais Samia.

..........................

Tufuatilie zaidi kupitia#

instagram @mainfmtanzania

#facebook @mainfmtanzania

#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab