National News

DKT. MPANGO AAGIZA MCHAKATO WA UJENZI KIWANDA CHA NGANO NJOMBE KUANZA

Tarehe: 28 Oct, 2023


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameziagiza wizara zinazohusika katika mnyororo wa kuchakata na kuzalisha Ngano kukutana na kuanza mchakato wa Ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata Ngano katika Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Dkt. Mpango ametoa maagizo hayo mara baada ya kupokea ombi la wakulima wa ngano katika wilaya hiyo la kujengewa kiwanda cha kuchakata zao hilo ili kuliongezea thamani.

Hayo yamejiri wakati Dkt. Mpango akiongea na wakazi wa Makete baada ya kuzindua mradi wa KKKT wa umeme wa Ijangala minihydro plant uliogharimu Bilioni 3.8 utakaozalisha Kilowati 360 za umeme.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab