National News

MAIN FM YAPONGEZWA KWA KUSAIDIA UTATUZI KERO YA VIFUSI KAGONGO, KIGOMA

Tarehe: 25 Oct, 2023


Wananchi katika Kijiji cha Kagongo, kata ya Kagongo Halmashauri ya Kigoma wameishukuru na kuipongeza Main Fm kwa kuwapazia sauti juu ya vifusi vilivyokuwa katika barabara iliyokuwa ikitengenezwa  katika kijiji hicho.

Kupitia kipindi cha Siku Mpya kinachoruka kupitia Main Fm kila siku za Jumatatu - Ijumaa kuanzia saa 12:00 - 10:00 Asubuhi baadhi ya wananchi wa  kijiji hicho waliwasilisha kero ya uwepo wa vifusi ambavyo havijasambazwa kwa muda vilivyokuwa vinaleta usumbufu na kero kwa watumiaji wa barabara hiyo wakiwemo bodaboda na watembea kwa migu katika barabara iliyokuwa inatengenezwa kutoka Kahabwa - Kagongo - Mgaraganza.

Baada ya kupokea taarifa hiyo Kipindi cha Siku Mpya kilifanya jitihada za kumtafuta Meneja wa TARURA Wilaya ya Kigoma Eng. Paul Mutapima ambaye alithibitisha uwepo wa vifusi hivyo na kukiri kwamba vifusi hivyo havijasambazwa kwa sababu ya taratibu za upimaji wa vifusi hivyo ambazo zilikuwa zinaendelea.

Mapema wiki hii mmoja wa wakazi katika kijiji hicho alituma salamu za Shukrani kupitia kipindi cha Siku Mpya kwa kuwapazia sauti juu ya kero hiyo ambayo tayari imeanza kutatuliwa.
...............
Tufuatilie zaidi
Instagram @mainfmtanzania
Facebook @mainfmtanzania 
Twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab