National News

MAKONDA KATIBU MKUU MPYA HALMASHURI KUU CCM TAIFA ITIKADI NA UENEZI

Tarehe: 22 Oct, 2023


Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 22 Oktoba, 2023 mjini Dodoma, katika kikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Suluhu_Suluhu_Hassan, pamoja na masuala mengine, imefanya mabadiliko madogo ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kwa kumteua Ndugu Paul Makonda kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, akichukua nafasi ya Ndugu Sophia Edward Mjema ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Wanawake, Watoto na Makundi Maalum.

Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imeridhia kwa kauli moja  kuielekeza Serikali kuendelea na hatua ya utiaji saini mikataba ya uendelezaji a uwekezaji wa bandari.

Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pia imemteua Ndugu Rabia Abdallah Hamid kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), akichukua nafasi ya Ndugu Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab