National News

RAIS SAMIA ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI SHEREHE ZA UHURU NCHINI ZAMBIA

Tarehe: 21 Oct, 2023


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Jamhuri ya Zambia ambazo zinatarajiwa kufanyika Oktoba 24, 2023 ambapo Viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika wanatarajiwa kuhudhuria maadhimisho hayo.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba amesema kuwa Rais Samia amealikwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema.

Kufuatia mualiko huo Rais Samia pia atafanya ziara ya kitaifa nchini humo kuanzia Oktoba 23 - 25 Mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine amepewa heshima ya kuhutubia Bunge la Jamhuri ya Zambia Oktoba 25 na atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Biashara kati ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Zambia.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab