National News

18 WAFARIKI HUKU 35 WAKIJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI NA LORI TABORA

Tarehe: 21 Oct, 2023


Watu 18 wamefariki dunia na wengine 35 kujeruhiwa baada ya Basi la Kampuni ya Alfa ambalo lilikuwa likitokea Mwanza kuelekea Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na Lori la mafuta kampuni ya GBP katika kijiji cha Undomo Wilayani Nzega mkoani Tabora.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Richard Abwao amesema waliofariki ni wanaume 13 na wanawake 5 huku chanzo cha ajali hiyo ikiwa ni dereva wa lori kulipita basi bila kuchukua tahadhari.
.........................
Tufuatilie zaidi kupitia
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab