National News

HIFADHI YA NGORONGORO YAIBUKA MSHINDI KIVUTIO BORA CHA UTALII AFRIKA

Tarehe: 16 Oct, 2023


Hifadhi ya Ngorongoro imetangazwa kuwa mshindi katika kipengele cha kivutio bora cha utalii barani Afrika (African leading tourist Attractions) na kupewa tuzo na mtandao wa World Travel Awards.

Tuzo hiyo imetolewa usiku wa Oktoba 15, 2023 katika hotel ya Atlantis The Royal Dubai nchi za Falme za Kiarabu ambapo Ngorongoro imeshinda tuzo hiyo baada ya kushinda vivutio vingine vya utalii barani Afrika ambavyo ni Table Mountain, Hartbeespoort aerial cableway, V& A Waterfront, Ruben Island vya afrika kusini, Ziwa Malawi, Okavango Delta ya Botswana, Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Pyramids of Giza ya Misri.

Meneja wa huduma za Utalii NCAA Bw. Peter Makutian alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya uongozi wa Shirika.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab