National News

MTOTO AFARIKI AKIOGELEA BWAWANI KIGOMA

Tarehe: 02 Oct, 2023


Mtoto mmoja anaekadiriwa kuwa na umri kati ya mika 10 hadi 12 ambaye jina lake halijafahamika amefariki wakati akiogolea katika bwawa lililopo eneo la Katosho katika mtaa wa Butunga kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma

Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa Mtaa huo wa Butunga Bw. Hamis Yassin Kalimwabu amesema kuwa alipokea taarifa kutoka kwa mlinzi wa kitalu cha Michikichi karibu na eneo hilo Bw. Rajab Haruna majira ya saa mbili na nusu asubuhi akimweleza kuwa kuna mtoto anaonekana akielea katika bwawa hilo ndipo mwenyekiti alifanya taratibu za kutoa taarifa kwa Diwani wa kata ya Kibirizi pamoja na polisi kwa ajili ya hatua zaidi.

Aidha mwenyekiti huyo amesema kuwa hadi wanakamilisha tukio la kuuopoa mwili huo ndugu wa marehemu huyo walikuwa bado hawajajulikana na taratibu za kutangaza matangazo katika vitongoji na sehemu mbalimbali ili kuwapata wazazi wa marehemu huyo zinaendelea

"Hadi sasa tumeendelea kutafuta na kutoa matangazo vitongoji mbalimbali na sehemu mbalimbali hatujapata wazazi wa marehemu huyo, kwa maelekezo ya OCCID na OCS Othman  mwili unapelekwa Hospitali ya Mkoa kwaajili ya kwenda kuhifadhiwa kuendelea kuwatafuta wazazi wa marehemu huyo". Alisema mwenyekiti

Tufuatilie zaidi
Instagram @mainfmtanzania
Facebook @mainfmtanzania 
Twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab