National News

WALIMU WAPEWA MOTISHA NA MURUGENZI MANISPAA KIGOMA/UJIJI

Tarehe: 25 Sep, 2023


Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi.Mwantum Mgonja ametoa motisha ya fedha kwa Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu ambao Shule wanazozisimamia  zilipata ufaulu wa matokeo ya juu kwa kipindi cha Mwaka 2022.

Motisha hizo amezitoa katika kikao kazi kilichofanyika  Leo Septemba 25, 2023 katika ukumbi wa Manispaa hiyo kikihudhuriwa na Maafisa Elimu Kata (19), Wakuu wa Shule( 33)na Walimu Wakuu (19).

Viongozi wa elimu waliopokea Motisha kutoka kwa Mkurugenzi ni pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari  Kichagachui na Mlole , Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kiezya na Buronge.

Katika kikao hicho Mkurugenzi  amewataka Viongozi wa elimu ngazi ya Kata na Shule kusimamia suala la Ufundishaji na Ujifunzaji wenye Matokeo, kusimamia maadili ya Wanafunzi na Walimu na kufanya vikao vya tathimini mara kwa mara juu ya maendeleo ya Kitaaluma.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab