National News

RC ANDENGENYE ASISITIZA UMAKINI UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO

Tarehe: 25 Sep, 2023


 

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewasisitiza watendaji wa serikali mkoani Kigoma kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa makini na uadilifu ili kutokuwa kikwazo kwa serikali katika kufikisha huduma kwa wananchi

 

Andengenye ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya BOOST na SEQUIP katika halmashauri ya Mji wa Kasulu huku akisisitiza ufuatiliaji na ufanyaji wa tathmini wakati wote wa utekelezaji wa miradi hiyo

 

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa watendaji wanapaswa kuepuka kuzipa nafasi changamoto yaliyowekwa na kuwataka wawe wawazi na kutumia mbinu shirikishi katika kutafuta suluhisho la changamoto hizo

 

Katika ziara hiyo Andengenye ametembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa ajili ya uboreshaji mazingira ya ufundishaji na kujifunzia chini ya program za BOOST na SEQUIP katika shule ya sekondari Nyumbigwa Mpya,Muka,Msambara Pamoja na shule ya msingi Kasulu,Nyasha na Kibagwe

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab