National News

TISA WAFARIKI KWA AJALI YA GARI MBEYA

Tarehe: 23 Sep, 2023


Watu 9 Wamefariki na wengine 23 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea  kwenye Mteremko wa Iwambi Mkoani Mbeya baada ya Lori aina ya Howo la Zambia kuligonga kwa nyuma Basi dogo aina ya Mitsubish Rosa ambapo chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Lori kushindwa kulimudu gari na kwenda kuligonga Basi hilo

Katika ajali hiyo waliopoteza maisha ni Wanaume (5) na Wanawake (4) huku waliojeruhiwa wakiwa ni Wanaume (13) na Wanawake (10).

Katika ajali hiyo dereva wa lori amekamatwa na atafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab