National News

MKURUGENZI HALMASHAURI YA BUSEGA ASIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGUZI

Tarehe: 22 Sep, 2023


Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Mohamed Mchengerwa (Mb) amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Busega mkoani Simiyu Veronica Vicent Sayore ili kupisha uchunguzi

Hatua hiyo inakuja baada ya Mchengerwa kupokea malalamiko kuhusu utendaji kazi usiyoridhisha ,kutokuwa na ushirikiano na viongozi wenzake  Pamoja na kutowashirikisha watendaji katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo

Pia Waziri Mchengerwa  amewataka wakurugenzi wa halmashauri nchini kusimamia dhana ya ushirikishwaji wa viongozi,watendaji na wananchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo Pamoja na kuimarisha mahusiano mazuri baina ya viongozi na watendaji ili kujenga timu yenye umoja katika kutekeleza jukumu la kuwahudumia wananchi

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab