National News

"MAJAJI NA MAHAKIMU 33 WAMEFUKUZWA KAZI KATI YA 2015 HADI 2019"- PROF. JUMA

Tarehe: 14 Sep, 2023


Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma ameeleza kuwa kati ya mwaka 2015 hadi 2019 majaji na mahakimu waliofukuzwa kazi kwa kukiuka nidhamu walikuwa 33, waliostaafishwa kwa ajili ya maslahi ya umma walikuwa 38, huku 13 wakipewa onyo na 15 walirejeshwa kazini.

Ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam katika uapisho wa majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama kuu pamoja na viongozi wengine walioteuliwa na Rais Samia.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab