National News

RAIS SAMIA AWATAKA MAJAJI KUSIMAMIA HAKI

Tarehe: 14 Sep, 2023


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka majaji kusimamia Haki na sio kuipindisha kwa pesa kidogo wanayopewa kwani ni kinyume na sheria.

Ameyasema hayo leo 14 Septemba,2023 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama kuu pamoja na viongozi wengine aliowateua kushika nyadhifa mbalimbali serikalini.

"Hakikisheni mnasimamia haki za watu, mwenye haki aipate, unajua suala la kutoa haki ni la Mungu peke yake, sasa kama Mungu amekujalia umeteuliwa kusimamia haki za wanadamu wenzio unafanya kazi inayofanana hapo, kasimamieni haki sababu mmeapa na mmeshika vitabu mnavyoviamini, mtakwenda kuulizwa kwanini ulipindisha haki kwa pesa chache ambayo ukitumia hata mwezi haufiki, hata kama utajenga lijumba la fahari halafu si utakufa utaliacha, na ukiliacha watoto wako wanauza"-   Amesema Rais Samia.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab