Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya serikali iliyoko madarakani mashariki mwa nchi ya Libya amesema zaidi ya watu 3,800 wameangamia katika mafuriko huko Derna, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo
Kulingana na msemaji huyo, Luteni Tarek al-Kharraz, hadi kufikia sasa vifo 3,840 vimerekodiwa katika jiji hilo ambapo miili 3,190 tayari imezikwa huku wageni 400, hasa Wasudan na Wamisri wakiwa ni miongoni mwa wahanga.
Pia ameongeza kuwa takriban miili 250 ilipatikana siku ya Jumatano, huku zaidi ya watu 2,400 wakiwa bado hawajapatikana