National News

DARASA LA SABA KUANZA MITIHANI LEO

Tarehe: 13 Sep, 2023


Wanafunzi wa Darasa la Saba wanatarajiwa kuanza mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi leo huku jumla ya watahiniwa 1,397,370 wakitarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu hiyo.

Akizungumza kuelekea mitihani hiyo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Said Ally Mohamed amewataka watu wote wanaohusika na mitihani hiyo kuzingatia sheria na kujiepusha na aina zote za udanganyifu.

"Tunaamini wanafunzi wameandaliwa vyema katika kipindi chote cha miaka saba, hatutegemei kuona watahiniwa wanafanya udanganyifu kwa kuwa tutawafutia matokeo, Si kitu tunachokipenda kuona mtoto amesoma miaka saba halafu anafutiwa matokeo". Amesema Dkt. Mohamed.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab