National News

SITA MBARONI KWA TUHUMA ZA WIZI WA VIFAA

Tarehe: 12 Sep, 2023


Jeshi la polisi mkoni kigoma limewakata watuhumiwa sita wa matukio ya uvunjaji na wizi wakiwa na mali mbalimbali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi wakiwa hawana nyaraka halali za umiliki.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma ACP Filemon Makungu amezitaja mali hizo ni pamoja na Televisheni mbili (2) flat screen na Televisheni moja ya chogo, visimbuzi viwili (2), simu saba (7) smartphone, simu ndogo tatu (3) ambapo watuhumiwa watafikishwa  mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika

Aidha jeshi hilo la polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja akiwa na  pikipiki moja (1) aina ya Boxer ambayo imekuwa ikitumika katika matukio ya uporaji wa mikoba na simu ambapo mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika

Sambamba na hayo pia wamefanikiwa kukamata pikipiki moja (1) ambayo ilitelekezwa na mtuhumiwa ambapo jitihada za kumtafuta mtuhumiwa huyo zinaendelea  ili achukuliwe hatua za kisheria

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab