Sports

MANDONGA AKALISHWA NA WANYONYI

Tarehe: 23 Jul, 2023


Bondia wa Kenya, Daniel Wanyonyi ameshinda pambano la marejeano dhidi ya Bondia Mtanzania, Karim Mandonga lililofanyika katika Ukumbi wa Sarit Expo Center jijini Nairobi, Kenya usiku wa kuamkia leo.

Wanyonyi ameshinda pambano hilo baada ya kupata pointi zote za majaji watatu (100-80, 100-80 and 100-89) waliokuwa wakiamua mchezo huo.

Mapema mwanzoni mwa mwaka huu Karim Mandoga alishinda pambano lake dhidi ya Bondia  huyo Wanyonyi kwa TKO katika raundi ya 5 ambapo pambano lilipotakiwa kuendelea raundi ya 6 Wanyonyi alikataa kurudi ulingoni kuendelea na pambano hivyo ushindi ukaenda kwa Mandonga.  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab