KIGOMA UJIJI KUONDOA VYOO VYA SHIMO SHULE ZA MSINGI
Tarehe: 10 Nov, 2026
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imetangaza mpango wa kujenga vyoo bora katika shule za msingi na maeneo ya umma, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuondoa matumizi ya vyoo vya shimo katika manispaa hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, Juma Hamsini, amebainisha hayo katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani, ambacho ni kikao chake cha kwanza tangu kuteuliwa kuiongoza manispaa hiyo.
Amesema kwa kuwa Kigoma Ujiji ni eneo la mjini, haipendezi shule za msingi na maeneo ya umma kuendelea kutumia vyoo vya shimo, hivyo kuna umuhimu wa kujenga vyoo bora vinavyoendana na hadhi ya manispaa hiyo.