National News

WITO WATOLEWA KWA WANASIASA KUFANYA MIKUTANO YENYE TIJA

Tarehe: 11 Sep, 2023


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini kutumia mikutano ya hadhara kutoa hoja fikra zenye tija zinazolenga kuimarisha utendaji serikalini.

Rais ametoa wito huo leo wakati akifungua mkutano wa Baraza maalum la Vyama vya Siasa kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab