MAIN PESA LOTTO YAZINDULIWA, WATANZANIA KUJISHINDIA MAMILIONI
Tarehe: 23 Sep, 2026
Kampuni ya Mainstream Group kwa kushirikiana na taasisi ya bahati nasibu ya taifa ITHUBA, chini ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, imezindua bahati nasibu mpya inayojulikana kama Main Pesa Lotto, inayolenga kuwapa Watanzania nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mainstream Group, Deogratius Mosha, amesema mchezo huo unatoa nafasi ya kujishindia zawadi papo hapo, ikiwemo fedha taslimu zitakazotolewa kwa washindi kila baada ya saa tatu.
Amesema droo za kupata washindi zitachezeshwa kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 3:00 usiku, huku mshiriki akiwa na nafasi ya kushinda kwa kutumia shilingi 1,000 pekee.
Mosha amesema mshiriki anaweza kuingia kwenye mchezo huo kupitia menyu ya mtandao wowote wa simu, kuchagua sehemu ya kulipa bili, kisha kuweka namba ya kampuni 711777, kumbukumbu ya malipo 123, na kiasi cha shilingi 1,000.
Amesema kwa kushiriki kwa kiasi hicho, mshiriki ataingia kwenye droo tatu ndani ya wiki moja, zitakazompa nafasi ya kujishindia mamilioni ya fedha.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Bahati Nasibu Tanzania, Mark Wahome, amesema wamechagua kushirikiana na Main FM kwa lengo la kuwafikia Watanzania wengi zaidi na kuwapa fursa ya kujishindia zawadi kupitia mchezo huo.