KATIBU TAWALA MKOA KIGOMA AHIMIZA USHIRIKIANO ZOEZI LA CHANJO YA POLIO
Tarehe: 08 Sep, 2023
Katibu Tawala mkoa wa Kigoma Albert Msovela amewaomba wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wanasiasa na wataalam wa afya mkoani Kigoma kushirikiana katika kampeni ya kutoa elimu ya chanjo ya Polio.
Akizungumza katika kikao cha kamati ya Afya Msingi mkoa, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye, Msovela amesema kuwa viongozi pamoja na wadau mbalimbali wanatakiwa kushirikiana katika kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuhusiana na zoezi hilo la kutoa chanjo linalotarajiwa kuanza tarehe 21-24 Septemba mwaka huu.
Kwa upande wake Mratibu Msaidizi wa chanjo mkoa wa Kigoma Deltus Sevelin amesema kuwa malengo waliyowekewa kwa mkoa ni kuwafikia watoto 880,084 huku kila halmashauri ikiwekewa malengo ya idadi ya watoto wanaotakiwa kuwafikia na kubainisha kuwa wamepokea dozi 1,100,500 kwa ajili ya zoezi hilo.