FUNDI BOMBA ARUDISHA DHAHABU ZA BILIONI 26 ALIZOZIFUKUA SITE
Tarehe: 17 Aug, 2026
Kijana mmoja kutoka nchini Ubelgiji anayefahamika kama Kobe alikuwa akifanya kazi ya mabomba kwenye nyumba ya Zamani ambayo kwa sasa haikaliwi na mtu, lilikuwa likimikikiwa na Familia ya kitajiri ya Van Assche mwishoni mwa Karne ya 19, ambapo kwa sasa Jengo hilo lipo chini ya Shirika la kijamii la Caw Oost-Vlaanderen.
Wakati akiendelea kuchimba baadhi ya sehemu kwenye nyumba hiyo aligundua dhahabu yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 10 ambayo ni sawa na Bilioni 26 za Kitanzania. iliyofichwa ndani ya ukuta.
Kijana huyo mwanzoni alifikiri ni sarafu za Euro 1, lakini baada ya kuona nuggati na mito ya dhahabu, akagundua ni hazina kubwa! Alipoona ukubwa wa dhahabu hizo akaamua kupiga simu polisi mara moja hakuwa na nia ya kuficha chochote. Sasa dhahabu ipo mikononi mwa serikali, na watafiti wanachunguza asili yake.