Sports
HARUNA CHANONGO ATAMBULISHWA RASMI MASHUJAA FC
Tarehe: 17 Aug, 2026
Klabu ya Mashujaa FC imemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji Haruna Chanongo kuwa mchezaji mpya wa kikosi hicho kwa msimu huu.
Chanongo anajiunga na Mashujaa FC akiwa sehemu ya mipango ya klabu hiyo katika kuimarisha kikosi chake, chini ya uongozi wa Kocha Mkuu Aman Josiah.
Ujio wake unatarajiwa kuongeza nguvu na ubunifu katika safu ya ushambuliaji ya Mashujaa FC, huku klabu hiyo ikijiandaa kwa msimu mpya wa mashindano.