KLABU YA MASHUJAA YAMTAMBULISHA MSHAMBULIAJI GEORGE MPOLE
Tarehe: 17 Aug, 2026
Klabu ya Mashujaa FC imemtambulisha rasmi mshambuliaji George Mpole kuwa mchezaji mpya wa kikosi hicho kwa msimu huu.
Mpole, ambaye aliwahi kutwaa tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania msimu wa 2021/2022, anarejea katika klabu hiyo kwa lengo la kuimarisha safu ya ushambuliaji na kusaidia timu kufanya vizuri katika msimu huu.
Mashujaa FC kwa sasa inanolewa na Kocha Aman Josiah, ambaye atakuwa na jukumu la kumtumia Mpole katika mipango ya kikosi hicho kuelekea msimu mpya.
Usajili huo unatarajiwa kuongeza nguvu katika kikosi cha Mashujaa FC, huku mashabiki wakisubiri kuona kama Mpole ataweza kurejesha makali yake ya ufungaji katika msimu huu.