Sports

RAIS WA MAREKANI TRUMP ATETEA INFANTINO ASIONDOLEWE FIFA

Tarehe: 11 Aug, 2026


#MICHEZO: Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema litakuwa “kosa kubwa” iwapo FIFA itafikiria kumuondoa Rais wake, Gianni Infantino ambaye anakabiliwa na ukosoaji kutoka kwa baadhi ya Mashirikisho ya Soka duniani. 


Trump amemtetea Infantino leo Agosti 11, 2026 kupitia Truth Social, akimtaja kuwa Kiongozi bora na akisema ameiongoza FIFA katika mafanikio makubwa ya Kombe la Dunia.

“FIFA itakuwa inafanya kosa kubwa sana ikiwa, kwa sababu yoyote ile, watafikiria kumuondoa Rais Gianni Infantino,” amesema Trump.

Kauli hiyo imekuja wakati Infantino akikabiliwa na ukosoaji kutoka UEFA, CONCACAF na AFC ambayo kupitia barua ya pamoja yamemtuhumu kuvunja uaminifu katika Uongozi wake. 

Mvutano huo umeongezeka baada ya Infantino kuanzisha mpango wa kuingiza uwekezaji binafsi katika mashindano ya FIFA, yakiwemo Kombe la Dunia, kabla ya kuuondoa kufuatia ukosoaji mkubwa.

FIFA kwa upande wake imetetea uongozi wake na kupinga kile ilichokitaja kuwa juhudi za kuidhoofisha Taasisi hiyo.