MAINSTREAM GROUP YASHINDA TUZO ZA TEHAMA KWENYE HUDUMA ZA FEDHA
Tarehe: 10 Aug, 2026
Mainstream Group Limited imeibuka Mshindi wa Pili (1st Runner Up) katika kipengele cha TEHAMA kwenye Huduma za Fedha (ICT in Financial Services) katika Tehama Awards 2026, kupitia VIKOBA App.
Kupitia chapisho lililotolewa na kampuni hiyo, Mainstream Group imesema tuzo hiyo ni utambuzi wa mchango wa VIKOBA App katika kuwawezesha wananchi kupata suluhisho za kifedha kwa njia ya kidijitali na kwa urahisi zaidi.
Kampuni hiyo imeeleza kuwa mafanikio hayo yamechangiwa na juhudi za timu yake, washirika pamoja na watumiaji wanaoendelea kuamini katika dira ya kampuni ya kukuza upatikanaji wa huduma jumuishi za kifedha.
Mainstream Group imesema itaendelea na safari ya kutumia teknolojia na ubunifu wa kidijitali katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa jamii.