Sports

PITSO MOSIMANE ATEULIWA KUWA KOCHA MPYA WA AFRIKA KUSINI

Tarehe: 08 Aug, 2026


Shirikisho la Soka la Afrika Kusini limethibitisha rasmi uteuzi wa aliyekuwa kocha wa Mamelodi Sundowns na Al Ahly, Pitso Mosimane, kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana.


Uamuzi huo umefikiwa na Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo baada ya majadiliano ya muda mrefu na Mosimane, ambaye kabla ya uteuzi huo hakuwa akifundisha timu yoyote.

Mosimane anarejea katika nafasi hiyo kuchukua mikoba ya Hugo Broos, ambaye ameiongoza timu ya taifa ya Afrika Kusini kwa kipindi cha miaka minne.

Kocha huyo mwenye uzoefu mkubwa katika soka la Afrika anatarajiwa kutumia uzoefu wake kuijenga upya Bafana Bafana na kuipa ushindani zaidi katika mashindano ya kimataifa.