Sports

MFUNGAJI BORA NBCPL MOSSI NDUWUMWE ATIMKIA MC ALGER

Tarehe: 07 Aug, 2026


Mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara  msimu wa 2025/26, Mossi Nduwumwe, ametangazwa kuwa mchezaji mpya wa klabu ya MC Alger ya Algeria akitokea Singida Black Stars.

Nduwumwe amejiunga na mabingwa hao wa Algeria kwa mkopo wa msimu mmoja, huku makubaliano hayo yakiwa na kipengele cha kumsajili moja kwa moja endapo atafanya vizuri.

Mshambuliaji huyo raia wa Burundi aliibuka kinara wa ufungaji wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2025/26 baada ya kufunga mabao 17, akitoa mchango mkubwa kwa Singida Black Stars na kuvutia klabu mbalimbali kabla ya kuhamia MC Alger.