National News

SEKTA BINAFSI NDIYO INJINI YA MAGEUZI YA UCHUMI - RAIS SAMIA

Tarehe: 05 Aug, 2026


#HABARI: Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali haiwezi peke yake kufanikisha mageuzi ya uchumi, hivyo imeiweka sekta binafsi kuwa mhimili mkuu wa ukuaji wa uchumi wa taifa.


Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 na Jukwaa la Miundombinu Afrika uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, Rais Samia amesema Serikali inalenga kuhakikisha asilimia 70 ya ukuaji wa uchumi unachangiwa na sekta binafsi, ikiwemo wawekezaji wa ndani na wa kimataifa.

Amesema jukumu la Serikali ni kuendelea kujenga mazingira rafiki na yanayotabirika kwa uwekezaji, kuwekeza katika miundombinu ya kimkakati na kuimarisha ushirikiano utakaowezesha sekta binafsi kuwekeza, kuleta ubunifu na kukuza ujasiriamali.

Rais Samia amesema katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imeendelea kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu, ikiwemo upanuzi na uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), pamoja na uwekezaji katika barabara, madaraja, korido za usafirishaji na viwanja vya ndege vya kisasa.

Ameeleza kuwa uwekezaji huo unalenga kuongeza ufanisi wa biashara, kupunguza gharama za usafirishaji, kuimarisha biashara na nchi jirani, na kuifanya Tanzania kuwa kitovu muhimu cha usafirishaji, biashara na uwekezaji barani Afrika.

Sikiliza MAIN FM kupitia 91.7 Mhz Kigoma, Kasulu, Uvinza, Buhigwe.

Pia tufuatilie kwenye Mitandao ya Kijamii, Instagram, Facebook, TikTok, na Youtube @mainfmtanzania pia tusikilize kupitia www.mainfm.co.tz pia Radio Box na Radio Garden tafuta Main FM

Fuatilia Youtube Chaneli Yetu ya Main FM Tanzania
#trending #viral #instagram #explorepage