Mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah, yuko njiani kuelekea Trabzon nchini Uturuki kwa ajili ya kukamilisha taratibu za uhamisho wake kwenda klabu ya Trabzonspor.
Salah ameonekana akiwa amevalia uzi wa Trabzonspor akiwa ndani ya ndege, huku akitarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo leo, Agosti 5, 2026.
Nyota huyo wa Misri amefikia makubaliano ya mwisho na Trabzonspor na anatarajiwa kuweka rasmi saini ya kujiunga na timu hiyo.