SIMBA YAFIKIA MAKUBALIANO YA KUMNASA NEO MAEMA KWA MKOPO WA MWAKA MMOJA
Tarehe: 05 Aug, 2026
Taarifa kutoka Afrika Kusini zinaripoti kuwa Simba SC imefikia makubaliano na klabu ya Mamelodi Sundowns ya kumsajili kiungo Neo Maema kwa mkopo wa mwaka mmoja kuelekea msimu wa 2026/27.
Maema, ambaye anatajwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaohitajika na kocha Steven Barker, anatarajiwa kurejea Simba kwa mkopo baada ya pande zote mbili kufikia mwafaka wa uhamisho huo.
Kiungo huyo alirejea Mamelodi Sundowns mwishoni mwa msimu uliopita na baadaye akaongezewa mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao wa Afrika Kusini, hatua iliyowapa nafasi ya kumruhusu tena kujiunga na Simba kwa mkopo.
Hadi sasa, Simba SC na Mamelodi Sundowns bado hawajatoa taarifa rasmi kuthibitisha makubaliano hayo.