RAPA SEAN "DIDDY" COMBS AONGEZEWA MUDA WA KIFUNGO BAADA YA KUPIGANA GEREZANI
Tarehe: 05 Aug, 2026
Rapa maarufu Sean "Diddy" Combs ameongezewa muda wa kifungo chake gerezani kufuatia tukio la kupigana na mfungwa mwenzake katika gereza analikotumikia adhabu.
Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, tarehe yake mpya ya kuachiliwa huru sasa imepangwa kuwa Februari 20, 2028, badala ya Januari 24, 2028 kama ilivyokuwa imeonyeshwa wiki iliyopita baada ya kupunguziwa kifungo.
Diddy alihukumiwa rasmi mwezi Oktoba 2025 kutumikia kifungo cha miezi 50 jela baada ya kupatikana na hatia katika makosa yanayohusiana na usafirishaji wa watu kwa shughuli za ukahaba. Mahakama ilimuondolea mashtaka mengine mazito yaliyokuwa yakimkabili.
Mabadiliko hayo ya tarehe ya kuachiliwa yamekuja baada ya kuripotiwa kuhusika katika ugomvi na mfungwa mwingine, tukio lililosababisha kuchukuliwa hatua za kinidhamu dhidi yake gerezani.