National News

TBA YAAGIZWA KUJENGA NYUMBA ZA BEI NAFUU

Tarehe: 07 Sep, 2023


Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa ameagiza Wakala wa Majengo (TBA) kuhakikisha wanakuja na mikakati itakayosaidia kujenga nyumba za bei nafuu hasa kwa vijana wanaoajiriwa katika utumishi wa umma ili kuweza kumudu gharama za maisha.

Bashungwa ameyasema hayo  mkoani Dodoma wakati alipofanya ziara yake kwa mara ya kwanza katika ofisi hizo na kuzungumza na menejimenti ya TBA ambapo amesisitiza uwekezaji wenye tija kwa watumishi na Taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Bashungwa ameagiza  (TBA), kuhakikisha inakusanya deni la Shilingi Bilioni 81.5 wanazodai kwa wapangaji wao ikiwa ni pamoja na  kuwaondoa wadaiwa sugu katika nyumba hizo  ili upatikanaji wa fedha wanazodaiwa  uweze kusaidia utekelezaji wa miradi mingine nchini.


  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab