MAASIFA USTAWI,MAENDELEO YA JAMII WASISITIZWA KUTOA ELIMU KWA WAZAZI KUHUSU MALEZI
Tarehe: 18 Nov, 2025
#KIGOMA:Maafisa maendeleo ya jamii na maafisa ustawi wa jamii katika Halmashauri za Mkoa wa Kigoma wametakiwa kutoa elimu ya malezi kwa jamii ili kuwajengea uelewa wazazi na walezi katika kuimarisha huduma ya Malezi Bora kwa watoto wao.
Wito huo umetolewa na katibu tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa wakati Akizungumza mjini Kasulu kwenye kikao kazi cha mafunzo ya wawezeshaji wa vikundi vya malezi na matunzo ya watoto kikijumuisha halmashauri zote 8 za mkoa wa Kigoma
Amesema ukuaji wa mtoto unategemea malezi bora kutoka kwa wazazi na Walezi, lishe bora pamoja na kuzingatia maadili mema yanayokubalika katika jamii.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Kigoma Bw. Msafiri Nzunuri amesema changamoto nyingi zinazowakumba watoto zinatokana na wazazi kutozingatia majukumu yao ipasavyo, jambo ambalo husababisha changamoto kwa watoto huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kutoa mafunzo ya malezi ili kukabiliana na changamoto hizo.
Afisa ameendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalumu Vaileth Mulyalya amesema wizara imeandaa sera ya malezi na imeahidi kuanzisha vikundi vya malezi inchi nzima ili kuimarisha ustawi wa Watoto.
Mtaalamu kutoka Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa mataifa UNICEF mkoa wa Kigoma Bi,Juliana Karusha amesema elimu ya malezi inayotolewa na maafisa maendeleo ya jamii imechangia kuongeza ufaulu wa wanafunzi na kukuza taaluma shuleni.