ZOEZI LA CHANJO KWA MIFUGO LAENDELEA HALMASHAURI YA MJI KASULU
Tarehe: 15 Jul, 2025
#KIGOMA:Halmashauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma imepokea zaidi ya dozi laki 3 kwa ajili ya Chanjo ya Kuku ikiwa ni kampeni ya Serikali kutambua takwimu na kutoa chanzo kwa mifugo.
Akizundua zoezi la chanjo kwa ngazi ya halmashauri ya mji wa Kasulu ambalo limefanyika katika kata ya Nyumbigwa, Katibu tawala wilaya ya Kasulu Bi.Theresia Mtewele amewataka wafugaji wa kuku,Kanga,mbuzi na Ng'ombe kuchanja mifugo yao ili kuimarisha usalama wa chakula.
Vilevile Bi.Mtewele ameeleza kuwa zoezi hilo hufanyika kila baada ya miaka mitano likiwa na lengo la kukuza soko la Biashara ya mifugo nje ya nchi na kukuza uchumi wa taifa katika sekta ya kilimo mifugo na uvuvi.
Mkuu wa idara ya kilimo mifugo na uvuvi, halmashauri ya mji kasulu Sabinus Chaula amesema uwepo wa magonjwa yanayoshambulia kuku hupelekea kifugo hiyo kupungua kwa wafugaji na kwamba zaidi ya dozi laki 3 za chanjo ya Kuku zitasaidia wafugaji kukuza uchumi wao kutokana na kwamba mifugo yao itakuwa katika hali nzuri.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Nyumbigwa Dorkasi Yohana ndagiwe na Anatolia Christopher wameshauri chanjo hizo kuendelea kutolewa mara kwa mara na kuwafikia wafugaji wengi kutokana umuhimu wa chanjo hiyo licha ya kushauri serikali kutoa chanjo hiyo kuanzia mwezi machi ili kutibu magonjwa ya kuku ambayo huibuka miezi kama hiyo na kusababisha hasara kubwa kwa wafugaji.