National News

UUHABA WA MAFUTA WASABABISHA FOLENI

Tarehe: 06 Sep, 2023


Foleni katika vituo mbalimbali vya kuuzia nishati ya mafuta imeendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo hali hiyo pia imeonekana Mkoani Kigoma katika baadhi ya maeneo ambapo watumiaji wa nishati hiyo wamesema kuwa imewaathiri katika shughuli zao za kila siku.

Wakizungumza na main Fm baadhi ya watumiaji wa mafuta hususani bodaboda waliokuwa wakisubiri kupata mafuta katika moja ya kituo cha kutolea huduma hiyo wamesema kuwa changamoto hiyo imewaathiri  katika shughuli zao za kila siku.

Moja ya mwananchi aliyekuwa katika foleni hiyo amesema kuwa kumekuwa na foleni kubwa ambayo inawafanya kukaa muda mrefu kusubiria huduma hiyo.

"Ni changamoto kubwa sana kwa sisi vijana yaani siyo asubuhi yaani tokea juzi mafuta tunakosa tunatafuta kigoma nzima tunakosa, kwahiyo sehemu ambapo kuna mafuta unakuta ni foleni kubwa sana unaanzia asubuhi mpaka jioni hujapata mafuta, unaona mpaka tunaamua kupaki pikipiki ndani unaona ndiyo changamoto tulizonazo sisi vijana hapa, kwahiyo sasa  hatujajua mafuta hamna au vipi na ukiangalia pikipiki saizi ni nyingi mitaani, unaona hazina mafuta"

Katika hatua nyingine wananchi hao wameiomba serikali kuwasaidia kutatua changamoto hiyo

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab