National News

MKUU WA MKOA KIGOMA AWAFUNDA WATUMISHI WA UMMA

Tarehe: 08 Jul, 2025


#KIGOMA:Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka watumishi wa Umma wilayani Kasulu kufanyakazi kwa weledi, uadilifu, nidhamu na kujituma ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi.

Balozi Sirro ametoa wito huo wakati akizungumza na watumishi wa umma viongozi wa dini pamoja na viongozi wa vyama vya siasa katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu.

Amesema watumishi wa umma wanatakiwa kuwajibikaji kwa kutimiza majukumu yao kwa ufanisi na uadilifu sambamba na kubainisha kuwa mafanikio ya serikali na ustawi wa wananchi yanategemea utendaji bora wa watumishi wa umma.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu amesema wilaya hiyo imeendelee kutafuta wawekezaji ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi huku akisisitiza kuwa hali ya usalama katika wilaya hiyo imeendelea kuimalika.

Mbunge wa Kasulu Mjini Profesa Joyce Ndalichako akizungumza kwa niaba ya wananchi wa wilaya hiyo amesema ujio wa mkuu wa mkoa wa kigoma umekuja na matumaini kwa wananchi utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Ziara ya Balozi Simon Sirro ni ya kikazi ya siku nne katika mkoa wa Kigoma, ambapo anatarajiwa kukutana na watumishi wa umma, kutembelea na kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo katika wilaya zote za mkoa huo.