SIRO AKABIDHIWA OFISI,ATAJA MAAGIZO ALIYOPEWA NA RAIS SAMIA
Tarehe: 03 Jul, 2025
#KIGOMA: Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amesema kuwa katika kufanikisha adhma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Mkoa wa Kigoma unafunguka kiuchumi na kuwa lango la biashara katika Mataifa yanayozungukwa na Ziwa Tanganyika ni lazima kuwekeza katika utalii wa vivutio mbalimbali mkoani Kigoma.
Balozi Sirro ameyasema hayo leo Julai 02, 2025 wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi ya mkuu wa Mkoa iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ikihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Mkoa huo Thobias Andegenye pamoja na Watumishi mbalimbali wa Mkoa wa Kigoma.
"Kigoma ni mkoa wa kimkakati wa kiuchumi, maana yake tukitambua ni wapi tunaweza kuweka vitega uchumi vyetu upande wa utalii hiyo ni fedha, tukikuza biashara yetu hiyo ni fedha na kwa kasi ya mkoa wetu kama tukienda hivi basi tutafika mbali zaidi" Balozi Sirro