HUDUMA VIPIMO VYA MIONZI IMEANZA HOSPITALI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI
Tarehe: 05 Jun, 2025
#KIGOMA:Huduma ya Utoaji wa huduma ya vipimo vya mionzi imeanza kutolewa kwa Wagonjwa wanaofika kupata matibabu katika Hospitali ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji iliyopo Kata ya Kagera.
Akitoa taarifa ya Utoaji wa huduma hiyo Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Dkt. Hashim Mvogogo amesema tayari vipimo kwa njia ya Mionzi imeanza kutolewa mara baada ya Mashine ya X-ray na Ultra Sound kufungwa.
Vilevile mganga huyo mkuu ametoa rai kwa Wananchi kufika hospitalini hapo kupata vipimo vya X-ray ya Kichwa, Miguu, tumbo, Mikono, kifua na mgongo huku akibainisha kuwa vipimo vya Utra sound pia vinatolewa kwa Watu wote ikiwa ni pamoja na wajawazito na kwamba baada ya vipimo mgonjwa atapata huduma za matibabu.