Entertainment

WANAMUZIKI WATANO WALIOPOTEA WAKUTWA WAMEFARIKI,GENGE LA UHALIFU LAHUSISHWA

Tarehe: 30 May, 2025


#MAREKANI:Wanamuziki watano wa kundi la Grupo Fugitivo waliopotea katika mji wa Reynosa, ulioko karibu na mpaka wa Marekani, wamethibitishwa kuuawa, huku washukiwa wakihusishwa na genge la ulanguzi wa dawa za kulevya.

Taarifa kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Jimbo la Tamaulipas, Irving Barrios Mojica, zinaeleza kuwa watu tisa wanaodaiwa kuwa wanachama wa genge la Gulf wanazuiliwa kwa uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo.

Kundi hilo la wanamuziki linasemekana kutoweka mnamo Mei 25 mwaka huu, walipokuwa safarini kuelekea kwenye tamasha la faragha.

Taarifa kutoka kwenye familia zao zzmeiripoti kuhusu kupokea vitisho na madai ya fedha za fidia baada ya kutoweka kwa wasanii hao.