#HABARI: Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma (KUWASA), kwa kushirikiana na Kampuni ya CollectTech Limited, imezindua mfumo mpya wa kiteknolojia uitwao Amanzi App unaolenga kuwezesha wananchi kutoa taarifa za mivujo ya maji moja kwa moja kwa mafundi kupitia simu janja.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Jenerali mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, amesema kuwa uzinduzi wa Amanzi App ni hatua kubwa katika kuboresha huduma za maji na kuhakikisha rasilimali hiyo muhimu haipotei.
Pamoja nayo amewahimiza wakazi wa Kigoma na Mamlaka nyingine nchini kutumia teknolojia hiyo kama suluhisho la tatizo la upotevu wa maji unaosababishwa na mivujo.