#MAIN FM CUP:Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua ameupongeza uongozi na kituo cha redio cha Main FM 91.7 Kigoma kwa namna kinavyoendelea kugusa maisha ya wananchi wa Kigoma katika sekta tofauti tofauti kwa kuandaa matukio yanayoiunganisha jamii na kuileta pamoja.
Pongezi hizo zimetolewa katika hafla ya uchezeshwaji droo ya timu shiriki za Main FM CUP iliyofanyika leo Mei 10, 2025 katika ukumbi wa Kigoma Social Hall manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo Dkt. Chuachua amepongeza jitihada zinazofanywa na kituo cha redio cha Main FM katika kuiunganisha jamii ikiwa ni pamoja na uendelezaji wa Ligi ya Main FM CUP inayokwenda kufanyika kwa msimu wake wa pili.
"Nitumie fursa hii kuwapongeza Main FM kwa kuendelea na Programu mbalimbali zinazoashiria utumishi wao kama sehemu ya wanakigoma nje ya shughuli za utangazaji na utoaji habari kwamba wana Programu mbalimbali wanazozifanya zinazogusa maisha ya wananchi wetu kwenye sekta mbalimbali" - Dkt. Chuachua