"ACHENI KUATAMIA KILA KITU KIZURI KUWA CHA KWENU"- ANDENGENYE
Tarehe: 09 May, 2025
#KIGOMA:Mkuu wa mkoa wa Kigoma Jenerali mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amewata wakuu wa taasisi mkoani hapa kuwawezesha watendaji walioko chini yao katika utekelezaji wa majukumu ili kuleta matokeo yanayotarajiwa katika taasisi zao.
Andengenye ameyasema hayo leo tarehe 9 Mei, 2025 wakati wa hafla ya ugawaji wa magari mawili yaliyotolewa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kwaajili ya ufuatiliaji na usimamizi wa utekelezaji wa shughuli za lishe mkoani Kigoma, ambapo ameongeza kuwa kumekuwa na baadhi ya wakuu wa taasisi ambao yanapoletwa magari mapya huyafanya kuwa ya kwao na kuwataka waachane na tabia hiyo na badala yake wajikite katika kuwawezesha walio chini yao kwasababu ndiyo wanaofanya kazi kwa kiasi kikubwa ili kuleta matokeo chanya.
Katika hatua nyingine amesisitiza kuwa endapo wafanyakazi hao hawatawezeshwa hawawawezi kuleta na kupata matokeo yanayotarajiwa huku akisisitiza kuwa magari hayo yaliyotolewa yakatumike kulingana na malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo.