National News

AFARIKI KWA KUANGUKIWA NA JIWE MGODINI

Tarehe: 05 Sep, 2023


Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Simon Charles mkazi wa Masanga Manispaa ya Kigoma Ujiji amefariki dunia baada ya kuporokewa na Jiwe wakati akichimba mawe katika eneo la Mgodi ambalo huwa linatumika na wachimbaji hao kujipatia kipato kupitia kazi hiyo

Akizungumza kwa njia ya simu na Main fm kuhusiana na tukio hilo Mwenyekiti wa Mtaa wa Masanga James Cherles Wlliam amesema kuwa jiwe hilo liliporomoka kutoka juu na kumwangukia mtu huyo na kupelekea kufariki na kuongeza kuwa kumekuwa na matukio kama hayo katika eneo hilo kwa zaidi ya mara moja hasa wakati wa masika
 
” Ukizingatia hilo siyo tukio kwamba ndiyo la kwanza, ni matukio yamekuwa yakijirudia mara kwa mara, hili hapa litakuwa tukio la tatu”. Amesema James.    

Akizungumzia kuhusiana na hali ya usalama katika katika aneo hilo Bw.James amesema kuwa watu wa madini wamekuwa wakizuia kwa kuifunga migodi ya mawe katika maeneo ambayo ni hatarishi kwa lengo la kulinda usalama wa waachimbaji

“Kimsingi usalama huwa wanakuja watu wa madini kuangalia ile migodi ambayo ni hatarishi inafungwa mpaka inapokuwa imekatwa  watu wanaruhusiwa kuendelea na kuchimba,kimsingi baada ya tukio la kwanza lile kutokea ile baadhi ya migodi iliyokuwa hatarishi ilikuwa inafungwa waanakuja wataalamu na maskaveta ya manispaa wanayakata yale mamigodi wakishayabomoa yale mamigodi ambayo ni hatarishi ndiyo watu wanaruhusiwa kwenda kuchimba”.Ameongeza mwenyekiti wa mtaa wa Masanga

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab