Sports

PARIS SAINT GERMAN YATINGA FAINALI KLABU BINGWA

Tarehe: 08 May, 2025


#MICHEZO: Timu ya Paris Saint-German imeifuata Inter Milan kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) baada ya ushindi wa jumla wa goli 3-1 dhidi ya Washika Mitutu, Arsenal.

Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa mzunguko wa  kwanza PSG walishinda 1-0 kabla ya kumaliza shughuli kwa kushinda 2-1 kwenye mchezo wa marudiano na kuwaondoa watetezi hao wa EPL.