#HABARI: Rais Donald Trump wa Marekani ametishia kwamba kutakuwa na "uharibifu mkubwa zaidi" kwenye Ukanda wa Gaza iwapo kundi la Hamas halitowaachia huru mateka wote wa Israel inaowashikilia.
Katika ujumbe kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth, Trump ameitaka Hamas kuwaachia mateka hao haraka iwezekanavyo pamoja na kukabidhi miili ya wale waliokufa akionya kwamba iwapo hilo halitofanyika kundi hilo litasambaratishwa.
Amesema hilo ni "onyo la mwisho" kwa kundi la Hamas akiapa kwamba ataipatia Israel kila inachohitaji "kumaliza kazi" kwenye Ukanda wa Gaza.
Tamko lake linafuatia onyo jingine la Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliyelitaka kundi hilo kuwakabidhi mateka wote wa Israel au likabiliwe na "madhara yasiyoweza kufikirika".