MAJAMBAZI WATATU WAUAWA WAKIJIBIZANA RISASI NA POLISI KIGOMA
Tarehe: 21 Feb, 2025
#KIGOMA:Jeshi la polisi mkoani Kigoma limewaua wahalifu watatu wa ujambazi baada kujeruhiwa katika tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha wakati wa majibizano ya risasi kati ya majambazi hao na askari polisi kwenye doria ya ya kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa tarehe 20 Februari, 2025 habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la polisi ACP Iddy Kiyogomo ameeleza kuwa tukio hilo limetokea Februari 20 mwaka huu katika eneo la Katundu Barabara ya Herushingo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ambapo Majambazi hao walikuwa wakifanya uhalifu huo kwa kutumia silaha kwa abiria baada ya kufunga Barabara.
Aidha katika tukio hilo kamanda Kiyogomo amesema kuwa wamefanikiwa kukamata silaha aina ya AK 47, Magazine 2 zikiwa na risasi 52, silaha za jadi Panga 2 na Marungu 2 na kwamba Majambazi hao watatu ambao hawajatambuliwa kwa majina wala anuani zao za makazi miili yao imehifadhiwa katika Hoispitali ya Wilaya ya Kasulu kwa utambuzi.
Sambamba na hayo jeshi la polisi limesema kuwa Majambazi hao walikuwa zaidi ya watatu waliouawa na wanaendeleaa na msako mkali kwa lengo la kuwabaini wengine huku likiwaaomba Wananchi, kujishughulisha na kazi halali za kujiingizia kipato zinazotambulika kwa mujibu wa sheria na kwamba jeshi hilo litaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa watu wote wanaojihusisha na uhalifu.