WATAALAMU, WADAU WA ELIMU KIGOMA WAPIGWA MSASA MDONDOKO WA WANAFUNZI
Tarehe: 20 Feb, 2025
#KIGOMA:Wataalamu na Wadau wa elimu Manispaa ya Kigoma/Ujiji wamepata mafunzo ya kufanya tathimini ya mdondoko wa Wanafunzi kwa Shule jumuishi.
Mafunzo hayo yamefanyika chini ya mradi wa Shule bora yakihudhuriwa na Maafisa Elimu, Wadhibiti ubora wa Shule, Maafisa maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa jamii wakiongozwa na Mdhibiti ubora wa Shule Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu Amosi Nkomali.
Akizungumza katika Mafunzo hayo kiongozi huyo amesema Shule za Msingi tisa (09) kati ya Shule 47 zina changamoto ya mdondoko wa Wanafunzi (kuacha/kukatiza masomo) hali iliyosabibisha kufanya tathimini ili kujua viashiria, na kuitaka jamii kukabiliana na tatizo hilo.
Amesema timu hiyo ya Wataalamu itakutana na Walimu, Wazazi na Kamati za Shule na kuweka mikakati ya kukabiliana na viashiria vya mdondoko wa Wanafunzi.